Albert Ojwang mwenye umri wa miaka 31, alikuwa mwanablogu na alikamatwa kufuatia machapisho yake katika mitandao ya kijamii yaliyokuwa yanamkosoa naibu inspekta mkuu wa polisi Eliud kipkoech Lagat.
Awali polisi ya Kenya ilisema alifariki katika seli yake baada ya kukigongesha kichwa chake ukutani.
Ila mpasuaji mkuu nchini humo Geoffrey Mutuma aliwaambia waandishi wa habari kuwa sababu ya kifo chake ilikuwa majeraha ya kichwa yaliyosababishwa na kupigwa na kifaa butu.
“Kulikuwa na majeraha mengi sana katika ngozi yake, mgongoni… yaliyotokana na kutumika kwa nguvu nyingi,” alisema Mutuma. “Ojwang pia alikuwa na kile tunachokiita, majeraha yanayotokana na kujitetea.”
Waandamanaji wamekusanyika katika chumba cha kuhifadhia maiti ulipo mwili wa Ojwang wakitaka majibu kutoka kwa polisi.
Kenya tayari ilikuwa katika hali ngumu wakati ambapo inaadhimisha mwaka mmoja tangu maandamano makubwa ya vijana nchini humo yaliyosababishwa na ngoza ya kodi na ufisadi, jambo lililosababisha polisi ya nchini humo kuingilia kati ambapo karibu watu 60 walifariki dunia.
Makundi ya kutetea haki za binadamu yanasema dazeni kadhaa za watu walishikiliwa na polisi baada ya maandamano hayo, huku wengi wakiwa bado hawajulikani wlaipo, na wengine wamekamatwa kwa makosa madogo madogo ya kuikosoa serikali na Rais William Ruto.