Mpango wa Ulaya wa kujibu mapigo kwa hatua ya upande mmoja ya Trump kuhusiana na vita vya Ukraine

Viongozi wa nchi za Ulaya wameamua kuchukua hatua zaidi za kuandaa mkakati wa kuwa na mpango huru na wa kujitegemea kiulinzi kufuatia msimamo na uamuzi wa upande mmoja uliochukuliwa na Marekani kuhusiana na vita vya Ukraine.