Mpango wa Trump kwa ajili ya Gaza; njama za kuifuta Palestina

Sayyed Abbas Araghchi, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria upinzani mkubwa wa nchi za eneo na kimataifa dhidi ya mpango haramu wa Rais wa Marekani kuhusu Gaza na kueleza kwamba, mpango huo wa kuwahamisha kwa nguvu watu wa Palestina kutoka Gaza kwa mujibu wa mpango wa kikoloni wa “kuifuta Palestina”.