Mpango wa nyuklia wa Iran: Mpatanishi kutoka Oman atangaza mkutano mpya wiki ijayo

“Mazungumzo yataendelea wiki ijayo, na mkutano mpya wa ngazi ya juu ulipangwa awali Mei 3,” Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman ameandika kwenye X, kufuatia duru ya tatu ya mazungumzo kati ya Iran na Marekani siku ya Jumamosi, Aprili 26.

Imechapishwa:

Dakika 3

Matangazo ya kibiashara

Marekani na Iran zilifanya duru ya tatu ya mazungumzo muhimu ya nyuklia nchini Oman siku ya Jumamosi, katika “mazingira mazito” kwa mujibu wa Tehran, baada ya majadiliano ya awali yaliyoelezwa kuwa ya kujenga na nchi hizo mbili, maadui kwa miongo minne. Majadiliano hayo, yaliyoanza asubuhi chini ya upatanishi wa Oman, yalifanyika “katika hali nzuri,” msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Iran Esmail Baghai amesema kwenye mtandao wa kijami wa X. Sasa yamemalizika na yataendelea wiki ijayo, mpatanishi wa Oman alitangaza siku ya Jumamosi.

“Mazungumzo yataendelea wiki ijayo, kukiwa na mkutano mpya wa ngazi ya juu uliopangwa hapo awali Mei 3,” Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman Badr al-Boussaïdi ameandika kwenye ukurasawake wa mtandao wa kijamii wa X, akiongeza kuwa “kanuni za kimsingi, malengo na masuala ya kiufundi (yalikuwa) yote yameshughulikiwa” wakati wa majadiliano ya hivi punde mjini Muscat.

Katika televisheni ya taifa, Waziri wa Mambo ya Nje Abbas Araghchi, ambaye anaongoza timu ya mazungumzo ya Iran, amesema kuwa “tofauti” zimesalia kati ya Washington na Tehran, “katika masuala makuu na maelezo.” Kwa upande wake, Marekani imekaribisha mijadala “chanya na yenye kujenga”. “Duru hii ya mwisho ya mijadala ya moja kwa moja na isiyo ya moja kwa moja ilichukua zaidi ya saa nne. “Bado kuna mengi ya kufanya, lakini maendeleo zaidi yamepatikana kufikia makubaliano,” afisa mmoja mkuu wa Marekani kwa sharti la kutotajwa jina lake amesema. “Tulikubaliana kukutana tena hivi karibuni huko Ulaya na tunawashukuru washirika wetu wa Oman kwa kuwezesha majadiliano haya,” ameongeza.

Kuzuia Iran kupata silaha za nyuklia

Mazungumzo hayo yanalenga kuhitimisha makubaliano mapya ya kuizuia Iran kupata silaha za nyuklia – matarajio ambayo Tehran imekuwa ikikanusha siku zote – badala ya kuondolewa vikwazo ambavyo vinadumaza uchumi wake, kufuatia kujiondoa kwa Marekani kwenye makubaliano ya kimataifa yaliyohitimishwa miaka mitatu mapema huko Vienna mwaka 2018, chini ya utawala wa kwanza wa Donald Trump.

Kikao cha mazungumzo ya kiufundi kati ya wataalamu kinatarajiwa kufanyika pamoja na majadiliano yanayoongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi na mjumbe wa Marekani katika Mashariki ya Kati Steve Witkoff, kupitia Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman, Badr al-Boussaïdi.

Kwa mujibu wa Baghai, uwezo wa kiulinzi wa Iran na mpango wa makombora ya balistiki haumo kwenye ajenda. “Mazungumzo yatazingatia masuala ya kiufundi na maelezo katika ngazi ya wataalamu” na yanaweza muda “kuongezwa ikiwa ni lazima,” shirika rasmi la habari la IRNA lilisema.

Mkutano wa awali wiki moja iliyopita ulielezewa kuwa “mzuri” na nchi zote mbili. “Ili mazungumzo yaendelee, lazima kuwe na onyesho la nia njema, umakini na uhalisia kwa upande mmoja kwensda upande mwingine,” Baghai alisema siku ya Ijumaa.

“Matumaini ya tahadhari”

Nchi za Magharibi zikiongozwa na Marekani na Israeli zinashuku Iran kutaka kupata silaha za nyuklia. Tehran inakanusha madai haya, ikitetea haki yake ya nishati ya nyuklia kwa madhumuni ya kiraia, haswa kwa nishati. Araghchi alionyesha kuwa nchi yake ilipanga kujenga vinu vipya 19, katika hotuba iliyorushwa kwenye mtandao wa kijamii wa X siku ya Jumanne.

Katika kulipiza kisasi kujiondoa kwa Marekani katika makubaliano ya Vienna, Iran imejitenga na makubaliano hayo, hasa kwa kurutubisha uranium hadi kiwango cha juu. Araghchi alielezea “matumaini ya tahadhari” ya nchi yake wiki hii kuhusu mchakato unaoendelea.

Tangu arejee katika Ikulu ya White House, Donald Trump amezindua upya sera yake inayoitwa “shinikizo la juu” dhidi ya Iran, akitaka ifanye mazungumzo mwezi Machi huku akitishia kuishambulia kwa mabomu ikiwa diplomasia itafeli. Katika taarifa zilizochapishwa siku ya Ijumaa na Jarida la Time, alihakikisha kwamba yuko tayari kukutana na kiongozi mkuu wa Iran au rais wa nchi hiyo. Wakati huo huo, Washington ilitangaza vikwazo vipya vinavyolenga sekta ya mafuta ya Iran siku ya Jumanne, huku Tehran ikilaani “mbinu ya uhasama”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *