Moto uliozuka majira ya saa mbili usiku wa kuamkia leo katika Kata ya Buseresere, Wilaya ya Chato – Geita umeteketeza maduka 10 …

Moto uliozuka majira ya saa mbili usiku wa kuamkia leo katika Kata ya Buseresere, Wilaya ya Chato – Geita umeteketeza maduka 10 …

Moto uliozuka majira ya saa mbili usiku wa kuamkia leo katika Kata ya Buseresere, Wilaya ya Chato – Geita umeteketeza maduka 10 yaliyokuwa na bidhaa mbalimbali.

Mashuhuda wa tukio hilo wameeleza kuwa waliona moto ukianza kwenye moja ya maduka yaliyokuwa yanauza vifaa vya umeme. Ndani ya muda mfupi, moto huo ulienea kwa kasi na kuyakumba maduka mengine yaliyokuwa jirani.

Jitihada za wasamaria wema kuuzima moto huo zilishindikana hadi kikosi cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kilipofika eneo la tukio na kushirikiana.

Baadhi ya wafanyabiashara hawakufanikiwa kuokoa mali zao kutokana na kasi ya moto, huku wengine wakifanikiwa kuokoa sehemu ya mali baada ya kufika mapema eneo la tukio.

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoni humo, Peter Nkwabi amesema chanzo cha moto huo bado hakijafahamika na uchunguzi unaendelea.

#AzamTVUpdares
✍Ester Sumira
Mhariri | John Mbalamwezi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *