
Urusi imetangaza Jumatatu, Juni 2, kwamba imezidungua ndege zisio kuwa na rubani 162 za Ukraine usiku wa kuamkia leo Jumatatu Juni 2. Nyingi mwa ndege hizo zimedunguliwa katika mikoa ya Kursk na Belgorod, inayopakana na Ukraine, huku mazungumzo mapya ya moja kwa moja kati ya Urusi na Ukraine yakitarajiwa kuanza mjini Istanbul.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
“Mifumo ya ulinzi wa anga imenasa na kuharibu ndege zisizo na rubani 162 za Ukraine” kati ya 11:10 jioni. na 5:00 usiku siku ya Jumapili, Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema katika taarifa iliyonukuliwa na shirika la habari la AFP.
Kulingana na DeepState, kikundi cha wachambuzi wa kijeshi wa Ukraine, jeshi la Urusi linazidisha mashambulizi yake kwenye mstari wa mbele: wastani wa mashambulizi ya kila siku yameongezeka kutoka 154.8 mwezi wa Aprili hadi 183.6 mwezi wa Mei, ongezeko kwa kiwango cha 19%. Siku iliyoshuhudiwa mashambulizi makali zaidi ilikuwa Mei 4, wakati Urusi ilizindua mashambulio 269. “Adui alikuwa imara na mwenye nguvu mapema na mwishoni mwa Mei, akijaribu kudumisha kiwango cha juu katika mashambulizi yake.”
Mnamo Mei 31, Oleksandr Syrsky, Kamanda Mkuu wa Kikosi cha Wanajeshi wa Ukraine, alisema kuwa jeshi la Urusi lilikuwa na nguvu zaidi kwenye mtari wa mbele wa Zaporizhzhia, ambapo kwa sasa linaendesha operesheni kali.