Gari moja limegonga umati wa watu huko Mannheim siku ya Jumatatu na kuua mtu mmoja na wengine kujeruhiwa vibaya, msemaji wa polisi wa Ujerumani amesema, huku akiongeza kwamba mshukiwa amekamatwa.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Mtu mmoja ameuawa na wengine kujeruhiwa vibaya katika mji wa Mannheim nchini Ujerumani baada ya gari kuwagonga watembea kwa miguu katikati mwa jiji siku ya Jumatatu (Machi 3). Polisi imetangaza kwamba imemkamata mshukiwa.
“Gari limegonga kundi la watu katika eneo la watembea kwa miguu huko Mannheim na mtu mmoja amefariki, watu kadhaa wamejeruhiwa vibaya,” msemaji wa polisi Stefan Wilhelm ameiambia televisheni ya NTV.
“Mshukiwa amekamatwa,” ameongeza, bila kutoa maelezo zaidi kuhusu sababu za tukio hilo, wala iwapo kitendo hicho kilikuwa cha makusudi au la.
“Tunaona tu watu waliojeruhiwa na mmoja aambaye amefariki, na hatujui la kufanya,” muuza duka alinukuliwa akisema na Gazeti la kila siku la Mannheimer Morgen. Ilikuwa ni siku ya katika eneo hili, katikati ya uzinduzi wa sherehe za Carnival katika mji huu wa magharibi mwa Ujerumani.
Mashambulizi kadhaa kwa kutumia magari katika miezi ya hivi karibuni
Katika miezi ya hivi karibuni, Ujerumani imekuwa ikikabiliwa na mashambulizi kadhaa ya magari ambayo yametikisa nchi.