Mmarekani Robert Francis Prevost anakuwa papa kwa jina Leo XIV

Mwishoni mwa siku ya pili ya kikao maalumu cha makadinali kwa uteuzi wa kiongozi mpya wa kanisa Katoliki duniani, moshi mweupe ulipanda kutoka kwenye bomba la moshi la Kanisa la Sistine siku ya Alhamisi, Mei 8 saa 12:09 saa za Ufaransa, ishara kwamba makadinali walikuwa wamemchagua papa mpya. 

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Kulingana na tangazo la Kadinali Protodeacon Dominique Mamberti, Kadinali wa Marekani Robert Francis Prevost anakuwa Papa Leo XIV, akimrithi Francis, ambaye alifariki Aprili 21. Papa wa kwanza kutoka Marekani, upapa wake unaweza kulenga nyanja ya kijamii ya Kanisa, kama jina lake linavyopendekeza.

Kardinali Robert Prevost ametangazwa kuwa kiongozi ajaye wa Kanisa Katoliki. Yeye ndiye Papa wa kwanza kutoka Marekani na kuchukua jina la papa Leo XIV.

Prevost ni mzaliwa wa Chicago nchini Marekani, na hadi kuchaguliwa kwake alikuwa akihudumu kama mkuu wa Dicastery wa kanisa kwa Maaskofu.

Papa Leo XIV mwenye umri wa miaka 69 ametumia muda wake mwingi akitumikia nchini Peru, na ana uraia wa Marekani na Peru.

Kanisa Katoliki limempata Kiongozi wake mpya, Papa Leo wa 14 atakayewaongoza takriban waumini bilioni 1.4 kote ulimwenguni. Kiongozi huyo amepatikana Alhamisi jioni baada ya uchaguzi uliofanywa na makadinali wapatao 133 kutoka mataifa 70.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *