Mmarekani Marc Fogel arejea Marekani nyumbani baada ya kuachiliwa na Urusi

Mmarekani Marc Fogel, ambaye alikuwa akizuiliwa nchini Urusi na kuachiliwa Jumanne, Februari 11, amerejea Marekani ambako alipokelewa na Rais Donald Trump.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

“Ahadii liyotokewa, yatekelezwa,” Ikulu ya Marekani imesema kwenye mtandao wa kijamii wa X, ikionyesha picha yake akishuka kwenye ndege. Wakati wa mahojiano yake na Marc Fogel, rais wa Marekani pia mehakikisha kwamba mfungwa mwingine ataachiliwa siku ya Jumatano, Februari 12.

Akizungumzia mabadilishano “ya haki, yenye busara” na Urusi ambayo yalisababisha kuachiliwa kwa mwalimu huyo wa Marekani, amesema kuwa “mtu mwingine ataachiliwa siku ya Jumatano,” bila kutoa maelezo yoyote.

Rais wa Marekani Donald Trump “alijadiliana katika mabadilishano yanayoonyesha nia njema ya Urusi na kuashiria kwamba tunaelekea katika mwelekeo sahihi ili kumaliza vita vya kutisha na vurugu nchini Ukraine,” serikali ya Marekani imesema katika taarifa yake, bila kutoa maelezo zaidi juu ya mazingira ya mazungumzo haya. Ni mjumbe maalum wa Donald Trump kwa Mashariki ya Kati, Steve Witkoff, ambaye aliandamana na Marc Fogel Ikulu ya White House imesema, ikiweka wazi ujumbe huu.

Marekani na Urusi mara kwa mara huzozana kuhusu raia wa kila mmoja kushikiliwa chini ya ulinzi wa kila mmoja. Hivi ndivyo ilivyokuwa mnamo mwezi wa Agosti 2024 wakati wa makubaliano makubwa zaidi ya kubadilishana wafungwa kati ya Urusi na nchi za Magharibi tangu enzi ya Vita Baridi, pamoja na kuachiliwa na Moscow kwa mwandishi wa Marekani Evan Gershkovich, mwandishi wa habari wa Urusi na mwenye asili ya Marekani Alsu Kurmasheva na mwanajeshi wa zamani Paul Whelan.