Mmarekani apatikana na hatia ya kumuua mtoto wa Kipalestina, Wadea Al-Fayoume

Baraza la majaji katika jimbo la Illinois nchini Marekani limemtia hatiani raia wa nchi hiyo kwa kosa la mauaji na uhalifu wa chuki katika tukio la Oktoba 2023 la kumchoma kisu na kumuua mtoto aliyekuwa na umri wa miaka 6 Mpalestina – Marekani, Wadea Al-Fayoume na kumjeruhi vibaya mama yake, Hanaan Shahin.