Mlipuko wa ugonjwa wa Mpox waukumba mji wa Kabare huku mzozo ukiendelea DRC

Mji wa Kabare, unaopatikana katika jimbo la Kivu Kusini umeathiriwa na mlipuko mkali wa ugonjwa wa Mpox, ugonjwa ambao kimsingi huambukizwa kupitia mgusano wa karibu wa ngozi hadi ngozi.