Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Beno Malisa, ametoa hamasa kwa wafanyabiashara mkoani Mbeya kuhakikisha wanakuwa na utamaduni mzuri wa …

Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Beno Malisa, ametoa hamasa kwa wafanyabiashara mkoani Mbeya kuhakikisha wanakuwa na utamaduni mzuri wa …

Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Beno Malisa, ametoa hamasa kwa wafanyabiashara mkoani Mbeya kuhakikisha wanakuwa na utamaduni mzuri wa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ili kuweza kutatua kero mbalimbali zinazohusu masuala ya kodi.

Kauli hiyo ameitoa wakati wa uzinduzi wa kampeni ya utoaji elimu ya kodi ya mlango kwa mlango wilayani humo, yenye lengo la kuhakikisha kwamba wafanyabiashara wanaelimishwa kuhusu masuala ya kodi, kutatuliwa kero zao za kikodi, na kujengewa mazingira rafiki ya kulipa kodi.

#AzamTVUpdates
✍Upendo Michael
Mhariri | John Mbalamwezi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *