Mkuu wa majeshi ya Iran: Umoja ndio njia pekee ya kukabiliana na utawala wa Kizayuni

Meja Jenerali Mohammad Bagheri Mkuu wa Majeshi ya Iran amesema kuwa, kwa kuzingatia dhati ya unyama na kupenda kujitanua utawala wa Kizayuni wa Israel, njia pekee ya kukabiliana na utawala huo vamizi na wa kigaidi ni mataifa ya eneo hili kudumisha umoja na mshikamano baina yao.