Mkuu wa jeshi la Uganda atishia kuushambulia mji wa Bunia mashariki mwa Kongo

Jenerali Muhoozi Kainerugaba Mkuu wa jeshi la Uganda jana aliandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X kuwa nchi hiyo itaushambulia mji wa Bunia mashariki mwa Kongo iwapo wapiganaji wote katika eneo hilo hawatasalimisha silaha zao katika muda wa saa 24.