Mkuu wa IRGC: Maadui wa Iran bado hawajapata vipigo ‘vikali’

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amepongeza uwezo wa kiulinzi na kijeshi wa Jamhuri ya Kiislamu na kusisitiza kuwa, maadui wa Iran bado hawajapata vipigo ‘vikali’ licha ya mashambulizi na operesheni kadhaa za kulipiza kisasi zilizofanywa katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.