Mkurugenzi wa hospitali ya Gaza ambayo imezingirwa na jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel ametoa wito kwa jamii ya kimataifa kuhitimisha maangamizi inayoendelea kufanywa na utawala huo kaskazini mwa Palestina.
Dakta Hussam Abu Safia, Mkurugenzi wa Hospitali ya Kamal Adwan huko Bahit Lahiya ametoa wito huo siku moja baada ya kujeruhiwa katika shambulio la anga la Israel katika hospitali hiyo.
“Kwa niaba yangu na wafanyakazi wa hospitali ya Kamal Adwan tunaiomba jamii ya kimataifa ichukue hatua. Tunaiomba WHO na taasisi nyingine za kimataifa kuchukua hatua haraka iwezekanavyo ili kutoa ulinzi kwa vituo na wafanyakazi wa tiba dhidi ya mashambulizi ya Israel”, amesema Mkurugenzi wa Hospitali ya Kamal Adwan.

Dakta Hussam Abu Safia amesema kuwa kila siku watu wa Gaza wanashuhudia mateso na mauaji ya kimbari ya Israel huku dunia ikiendelea kunyamaza kimya na mbele ya umwagaji damu huko kaskazini mwa Gaza.