Mkutano wa Lishe kwa Ukuaji: Ufaransa yachukua mwenge wa mapambano dhidi ya utapiamlo

Baada ya Japani mwaka 2021, Ufaransa inaandaa toleo la 3 la mkutano wa kilele wa Lishe kwa Ukuaji “Nutrition for Growth” huko Paris, tangu Alhamisi, Machi 27 na Ijumaa, Machi 28. Toleo hilo linalolenga kutoa msukumo mpya katika mapambano dhidi ya utapiamlo, ambayo tayari yameathiri watu bilioni 7 ulimwenguni kote. Mkutano huo tayari unalenga kukusanya dola bilioni 27 kwa ahadi za kujaribu kukomesha janga hili.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

“Mapambano kwa ajili ya amani na sayari yetu”: mbele ya hadhira ya viongozi na watu mashuhuri kama vile Mfalme wa Lesotho, pamoja na wawakilishi wengi wa mashirika ya kimataifa na wakfu waliokusanyika kwa ajili ya mkutano wa “Nutrition for Growth” – Lishe kwa Ukuaji, ambao unafanyika tangu Alhamisi, Machi 27 na Ijumaa, Machi 28 huko Paris, hivi ndivyo Emmanuel Macron alivyowasilisha umuhimu wa kupambana.

“Afya ya binadamu inategemea kile tunachokula, ubora wa udongo wetu, mimea yetu, wanyama wetu,” rais wa Ufaransa pia ameeleza, akitangaza katika hafla hii mchango wa dola bilioni 27 ili kutoa msukumo mpya katika mapambano haya – ahadi sawa na ile iliyotolewa Tokyo miaka minne iliyopita – akihimiza sekta ya kibinafsi kuhusika zaidi.

Ili kufikia kiasi hicho, wafadhili kadhaa wamejibu: Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), kwa ahadi ya ufadhili wa dola bilioni 9.3, Benki ya Dunia, kwa dola bilioni 5, na Umoja wa Ulaya, kwa dola bilioni 3.4, haswa. Wakfu nne za hisani, ikiwa ni pamoja na Gates Foundation na Eleanor Crook Foundation, wametangaza mchango wa dola milioni 250, hasa kuboresha lishe ya wanawake wajawazito.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *