Mkutano mwingine kati ya Ukraine na Marekani unaendelea mjini Riyadh

Mkutano mwingine kati ya timu za Ukraine na Marekani kuhusu usitishwaji vita kati ya Kyiv na Moscow unaendelea mjini Riyadh, chanzo cha ujumbe wa Ukraine kimeliambia shirika la habari la AFP siku ya Jumanne, Machi 25.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Mkutano mpya kati ya timu za Ukraine na Marekani kuhusu usitishwaji vitakati ya Kyiv na Moscow unaendelea mjini Riyadh, siku moja baada ya kumalizika kwa duru ya kwanza ya majadiliano kati ya Urusi na Marekani.

“Bado tunafanya kazi na Wamarekani,” chanzo hiki kimekiambia kikundi kidogo cha vyombo vya habari, ikiwa ni pamoja na AFP. Haya yanajiri baada ya mazungumzo marefu kati ya Marekani na Urusi siku moja kabla katika mji mkuu wa Saudi Arabia.

Mkutano mpya kati ya timu za Ukraine na Marekani kuhusu usitishwaji vitakati ya Kyiv na Moscow unaendelea mjini Riyadh, siku moja baada ya kumalizika kwa duru ya kwanza ya majadiliano kati ya Urusi na Marekani. 

Hakuna kutoa taarifa yoyote kuhusu mazungumzo

Hakuna kutoa taarifa yoyote kuhusu mazungumzo na Marekani, Kremlin imeonya, na kuongeza kuwa hakuna tarehe madhubuti iliyowekwa kwa majadiliano zaidi.

Umoja wa Mataifa kuhusshwa katika mazungumzo

Urusi inataka kuhusisha Umoja wa Mataifa katika mazungumzo na Marekani kuhusu uwezekano wa usitishwaji vita nchini Ukraine, mmoja wa wapatanishi wa Urusi, Grigory Karasin, ameliambia shirika la habari la Urusi la Tass siku ya Jumanne. “Tutaendelea” kuzungumza, “kwa kuhusisha jumuiya ya kimataifa, kwanza kabisa Umoja wa Mataifa na baadhi ya nchi,” ametangaza Bw. Karassine, seneta na mwanadiplomasia wa zamani, baada ya masaa kumi na mbili ya mazungumzo ya faragha siku moja kabla huko Saudi Arabia na wajumbe wa Marekani.

Mwisho wa mazungumzo jijini Riyadh

Baada ya mazungumzo ya faragha ya saa 12 nchini Saudi Arabia, Urusi na Marekani zilihitimisha majadiliano siku ya Jumatatu yaliyolenga kuasisi mapatano ya kiasi fulani nchini Ukraine. Ikulu ya White House na Kremlin zitatoa taarifa ya pamoja siku ya Jumanne.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *