TAARIFA KWA UMMA
Ofisi ya Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) inapenda kuwataarifu walimu na Watanzania wote kwa ujumla kuwa chama kinatarajia kufanya Mkutano mkuu wa saba utakaofanyika kwa muda wa siku mbili kuanzia 28 na 29 Mei Jijini Dodoma.
Pamoja na mambo mengine Mkutano Mkuu huo utafanya uchaguzi wa viongozi kwa nafasi mbalimbali kwa Ngazi ya Taifa
Hii ni baada ya kukamilika kwa chaguzi zilizokuwa zikiendelea nchini kote kwa ngazi za shule (Tawi), Wilaya na Mikoa na sasa chama kitakamilisha Ngazi ya Taifa.
Miongoni mwa nafasi za kitaifa zinazotarajiwa kufanyiwa uchaguzi ni pamoja na:-
i.Rais wa CWT
ii.Makamu wa rais CWT
iii. Katibu Mkuu wa CWT
Iv. Naibu katibu mkuu CWT
V.Mweka hazina CWT
Vi. Mwakilishi wa walimu wenye ulemavu
vii. Mwakilishi wa walimu vijana
Viii. Mwakilishi wa Walimu wanawake
ix.Mjumbe wa kamati ya utendaji TUCTA kutoka CWT
x.Wadhamini watatu
Xi. Vitengo mbalimbali vya chama
Chama kinawakaribisha wajumbe wa mkutano mkuu kushiriki tukio lao hilo muhimu na la kihistoria
Aidha orodha ya wagombea wa nafasi imetolewa kwa Umma.
Imetolewa na
JUMA A. DEDU – AFISA HABARI NA MAHUSIANO CWT HQ
The post MKUTANO MKUU WA SABA WA CWT KUFANYIKA MEI 28 NA 29,MWAKA HUU JIJINI DODOMA appeared first on Mzalendo.