Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme nchini (TANESCO), Lazaro Twange amewaomba wakuu wa mikoa na wilaya nchini kuongoza kwa k…

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme nchini (TANESCO), Lazaro Twange amewaomba wakuu wa mikoa na wilaya nchini kuongoza kwa k…

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme nchini (TANESCO), Lazaro Twange amewaomba wakuu wa mikoa na wilaya nchini kuongoza kwa kuwa mfano wa kutumia nishati mbadala ya kupikia ili kulinda mazingira kwa kuendana na malengo ya taifa ya kuhakikisha zaiid ya asilimia 80 ya wananchi wanatumia nishati safi ifikapo 2032.

Twange ametoa wito huo kwa wakuu wa mikoa baadhi ya wilaya za mikoa ya Kanda ya Ziwa alipowatembelea na kuwagawia zawadi za majibo mbadala ya kupikia.

“Majiko tuliyowapatia viongozi hawa yanatumia umeme kidogo na ni mfano bora kwa matumizi ya jikoni yatakayosaidia kuongeza uelewa kwa wananchi baada ya wao kuwa na uzoefu nayo” amesema Twange

Miongoni mwa wakuu wa mikoa waliopatiwa majiko hayo na elimu ya manufaa ya kutumia majiko hayo ya nishati mbadala ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Saidi Mtanda na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Kenan Kihongosi.

Wengine ni Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Julius Mtatiro.

Ziara hiyo ya Mkurugenzi wa TANESCO katika mikoa ya kanda ya ziwa imelenga kukagua miradi ya umeme na kuongeza msisitizo wa matumizi ya nishati safi ya kupikia ya umeme ikiwa ni muendelezo wa kampeni inayofanywa na shirika hilo kuchagiza ajenda ya serikali.

Mhariri @moseskwindi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *