Mkandarasi wa Kampuni ya China WU Yi Ltd amepewa jukumu la ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami kutoka Waso hadi Loliondo yenye urefu wa kilomita 10, wilayani Ngorongoro, mkoani Arusha.
Mkataba wa ujenzi huo umetiwa saini leo Juni 9, 2025 katika hafla maalum iliyofanyika kwa lengo la kuanza rasmi utekelezaji wa mradi huo muhimu kwa maendeleo ya wananchi wa eneo hilo.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, paul makonda amesema Serikali imeendelea kuwekeza katika miradi ya kimkakati ya miundombinu, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kufungua fursa za kiuchumi na kijamii kwa wananchi.
Ameongeza kuwa, usanifu wa barabara hiyo ulianza mwaka 2012, na sasa utekelezaji wake unaanza kwa kasi, ikiwa ni ishara ya dhamira ya serikali ya kuhakikisha huduma bora za usafiri na usafirishaji zinafikia maeneo yote ya nchi.
✍ @claud_jm
#AzamTVUpdates