Milipuko mikubwa yasikika Tehran, Israeli inadai kufanya “shambulio la mapema” dhidi ya Iran

Milipuko mingi mikubwa imesikika usiku wa Alhamisi, Juni 12 kuamkia Ijumaa, Juni 13 nchini Iran, haswa katika mji mkuu Tehran. Kufuatia hayo, chanzo cha jeshi la Israeli kimeripoti kuwa taifa hilo la Kiyahudi limelenga vituo kadhaa vya nyuklia vya Iran. Akitarajia jibu la Jamhuri ya Kiislamu, Waziri wa Ulinzi wa Israeli ametangaza hali ya hatari nchini humo.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Ikishuku kuwa Tehran inataka kupata silaha za nyuklia, Israeli imtangaza usiku wa Alhamisi, Juni 12 kuamkia Ijumaa, Juni 13 kwamba imefanya mfululizo wa kwanza wa “mashambulio ya mapema” dhidi ya malengo ya kijeshi ya Iran na nyuklia. Kwa mujibu wa chanzo cha kijeshi cha Israeli taifa la Kiyahudi limefanya “dazeni” za mashambulizi katika Jamhuri ya Kiislamu yote. Milipuko imesikika katika mji mkuu na katika eneo la kurutubisha uranium la Natanz katikati mwa Iran.

Kiongozi mwenye ushawishi kutoka kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi, Hossein Salami, ameuawa katika shambulio la Israeli, kwa mujibu wa mashirika ya habari ya Iran Tasnim na Mehr, huku televisheni ya taifa ikiripoti kuwa makao makuu ya kikosi hicho yaliteketea kwa moto na moshi ukifuka kutoka kwenye jengo hilo kwenye mtaa wa Pirouzi mashariki mwa Tehran.

Operesheni hiyo ya kijeshi, ambayo “awamu yake ya kwanza” jeshi la Israeli limetangaza kuwa imekamilika, itadumu “siku nyingi inavyohitajika,” ameonya Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu. Kwa upande wake, Waziri wa Ulinzi wa Israeli Israel Katz ametangaza kuwa hali ya hatari imetangazwa katika nchi nzima ya Iran, ambayo pia imefunga anga yake, ikihofia jibu kutoka kwa Iran.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani amesema kuwa Marekani haikuhusika katika shambulio la Israeli na akaionya Iran “kutolenga maslahi ya Marekani” kwa kulipiza kisasi. Katika taarifa, Marco Rubio amesema kwamba “kipaumbele” cha nchi yake ni kulinda vikosi vyake vilivyotumwa Mashariki ya Kati.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *