Mikoa 25 kupata mvua kubwa kuanzia leo

Dar es Salaam. Kama unaishi kwenye mikoa hii 25 nchini chukua hatua kwa kuwa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetabiri mvua kubwa itakayonyesha siku tatu kuanzia leo Machi 9, 2025.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Machi 8, 2025, TMA imesema hali hiyo itashuhudiwa kwenye baadhi ya maeneo ya mikoa hiyo kati ya leo hadi Jumanne ya Machi 11.

Mikoa iliyopewa angalizo ni Kigoma, Katavi, Tabora, Singida, Dodoma, Simiyu, Mara, Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Kagera, Geita, Mwanza na Shinyanga.

Mingine ni Tanga, Morogoro, Dar es Salaam, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia), Mtwara, Lindi, Rukwa, Mbeya, Iringa, Songwe, Njombe na Ruvuma pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.
“Kiwango cha athari zinazoweza kutokea ni wastani, baadhi ya makazi kuzungukwa na maji,” imeandikwa kwenye taarifa hiyo.