Miili ya wanandoa wawili waliofariki dunia wakiwa chumbani katika eneo la Tabata Bonyokwa Wilaya ya Ilala, inatarajiwa kuzikwa katika Wilaya ya Mwanga, mkoani Kilimanjaro, mara baada ya Jeshi la Polisi kukabidhi miili hiyo kwa ndugu wa marehemu.
Jeshi la Polisi bado linaendelea na upelelezi ili kubaini chanzo cha vifo hivyo.
Nini maoni yako juu ya tukio hili? Tuandikie na tutayasoma #AdhuhuriLive ifikapo saa 7:00 mchana kupitia #UTV.
#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi