Miili 10,000 ya Wapalestina inaaminika imefunikwa na vifusi, zoezi la ufukuaji limeshapata 100

Duru za tiba za Wizara ya Afya ya Palestina katika Ukanda wa Ghaza zimeripoti kuwa miili isiyopungua 97 imegunduliwa chini ya vifusi katika maeneo tofauti ya ukanda huo katika zoezi la ufukuaji lililoanza siku ya Jumapili baada ya kutekelezwa usitishaji vita.