
Mgogoro wa Kivu mbili, mashariki mwa DRC, sio mzozo mmoja, wala sio sababu moja, kama vile madini au mivutano ya kikabila. Inatokana na msukosuko wa mambo ya kihistoria, ardhi, usalama na kisiasa ambayo yanakuwa kwa zaidi ya miongo mitatu.
Imechapishwa:
Dakika 3
Matangazo ya kibiashara
Ni mgogoro ambao umedumu kwa miongo mitatu, huku wahusika wakuu wote wakionekana mara kadhaa katika mgogoro huo. Lakini kwa kweli, mizizi ya mgogoro katika sehemu hii ya DRC inarudi nyuma zaidi. Je, inawezekana kusema juu ya mgogoro mmoja, au migogoro kadhaa iliyoingiliana? Kinyume na hotuba zinazotawala, kila kitu hakiwezi kupunguzwa kwa suala la madini peke yake, kama baadhi ya viongozi huko Kinshasa wanapendekeza, wala kwa tatizo la ubaguzi dhidi ya Watutsi, ambalo mara nyingi hutolewa na Kigali.
Ni vigumu kujuwa ukweli hali wa mgogoro huu. Inategemea mienendo inayoingiliana, ya zamani, mara nyingi inayoingiliana ambayo huimarisha kila mmoja. Lengo hapa si kuandika upya historia, lakini kutoa funguo za kuelewa mivutano ya sasa katika mikoa miwili ya Kivu. Ili kufanya hivyo, tumelinganisha vyanzo kutoka kwa matukio ya sasa, kazi ya kihistoria na wataalam wanaofahamu vema historia ya nchi hii. Tunaweza kutambua angalau sababu kuu sita zinazounda mgogoro huu. Zimeunganishwa, wakati mwingine zimetofautiana, na zote huchangia kuongezeka au kuendelea kwa vurugu.
Idadi ya watu na siasa za suala la utambulisho
Mkoa wa Kivu ndio kitovu cha mabadiliko ya kipekee ya idadi ya watu. Kama vile mwanajiografia Mfaransa Roland Pourtier anavyoeleza, eneo hili linanufaika kutokana na mwinuko chini ya ikweta. “Ubaridi, jambo ambalo ni zuri kwa kilimo na ufugaji wa ng’ombe. Hii imevutia kwa muda mrefu watu wanaojihusisha na kilimo na ufugaji,” anasema. Matokeo yake, Kivu mbili sasa ni miongoni mwa maeneo yenye watu wengi zaidi barani Afrika.
Imeongezwa kwa msongamano huu wa asili historia tata ya wahamaji, hasa ile ya watu ktoka jamii ya Banyarwanda. Kulingana na Filip Reyntjens, mtaalamu katika Maziwa Makuu, baadhi ya watu hao walihama kutoka kusini-magharibi mwa Rwanda mapema katika karne ya 18. Kwa hivyo wana haki sawa kwa utaifa wa Kongo kama makundi mengine yaliyokuwepo kwa muda mrefu, kama vile Bashi au Banande.
Mwelekeo mwingine wa kuzingatiwa unaangaziwa na mwanajiografia Jean-Pierre Chrétien ambaye anakumbusha kwamba kuanzia miaka ya 1930, mamlaka ya Ubelgiji ilihimiza mtiririko mkubwa wa wahamiaji wa Wanyarwanda katika eneo hilo, hasa kaskazini-magharibi mwa Ziwa Kivu. Jason Stearns, mtafiti katika Kituo cha Ushirikiano wa Kimataifa katika Chuo Kikuu “Center on International Cooperation” cha New York, ambako anaongoza kikundi cha utafiti cha Kongo, anasema zaidi ya watu 150,000 kutoka Rwanda walihamishwa kati ya mwaka 1928 na 1956, hasa ili kukidhi mahitaji ya kazi katika shughuli za madini na kilimo za Ulaya, hasa katika eneo la Masisi, ambako watu kutoka jamii ya Hunde mara nyingi walikataa kufanya kazi.
Baada ya muda, takwimu zimeonekana kuwa muhimu: katika Masisi, msongamano uliongezeka kutoka wakazi 12 kwa kilomita mraba mwaka 1940 hadi wakazi 111 kwa kilomita mraba mwaka 1990, na idadi ya ng’ombe kutoka ng’ombe 21,000 mwaka 1959 hadi 113,000 mwaka 1983, kulingana na vyanzo mbalimbali. Ukuaji huu wa kasi umesababisha shinikizo kubwa kwa ardhi, na kufanya mashindano kuwa makali zaidi.
Mvutano wa kwanza wa kisiasa ulionekana mnamo mwaka 1958, wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa. Baadhi ya viongozi wa eneo hilo walikataa haki ya kupiga kura kwa wahamiaji ambao walikuwa wakiishi wakati wa ukoloni, ingawa walikuwa raia halali. Chini ya Mobutu (1965-1997), uteuzi wa wasimamizi wa nje wakati mwingine ulisaidia kupunguza uhasama wa ndani kwa muda.
Lakini ilikuwa mwaka wa 1991, na tangazo la sensa ya kitaifa, ambapo mvutano ulianza tena. Kinshasa ilibainisha kuwa “upandikizaji” wa kikoloni hautatambuliwa kama raia wa Zaire. Vurugu zilizuka, haswa dhidi ya vituo vya sensa huko Masisi. Vurugu ziliendelea hadi mwaka 1993, kabla ya kuwa mbaya zaidi baada ya mwaka 1994, na kuwasili kwa wakimbizi wa Kihutu milioni 1.5 kutoka Rwanda, ikiwa ni pamoja na baadhi ya askari wa zamani wa utawala wa Juvénal Habyarimana (1973-1994). Ujio huu ulivuruga uwiano wa ndani, ikiwa ni pamoja na kati ya Wahutu wa Kongo na Watutsi.
Filip Reyntjens anabainisha kuwa wakimizi hawa wapya walichochea uhasama huu: “Banyarwanda walionekana kama kundi moja, lakini baada ya mwaka , walijitambua tena kama Wahutu au Watutsi. “Katika eneo hili, anazungumzia “vitambulisho vinavyobadilika,” mara nyingi vinatumiwa na “wanaohatarisha usalama,” ambao pia ni wafanyabiashara. Idadi hii ya watu isiyo imara inaendelea kuwa sababu ya mgogoro hata leo.