Mhafamu Papa Francis, kiongozi wa kanisa Katoliki duniani, mtetezi wa wangonge aliyeaga dunia

Papa Francis ambaye kwa jina lake la asili ni Jorge Mario Bergoglio, alizaliwa huko Buenos Aires, Argentina, tarehe 17 Desemba 1936 – yeye ni mtoto mkubwa kati ya watoto watano. Wazazi wake walikimbia nchi yao ya asili ya Italia ili kuepuka maovu ya ufashisti.

Imechapishwa:

Dakika 2

Matangazo ya kibiashara

Alipenda mchezo wa tango (ngoma ya asili ya Argentina) na akawa shabiki wa klabu yake ya soka ya mtaani ya, San Lorenzo.

Alipona baada ya kuugua nimonia, na kufanyiwa upasuaji wa kuondoa sehemu ya pafu lake. Na hilo lilimuacha katika hatari ya kuambukizwa katika maisha yake yote.

Akiwa mzee pia alipatwa na maumivu kwenye goti lake la kulia, ambayo aliyataja kuwa ni “unyonge wa kimwili.”

Bergoglio akiwa kijana alifanya kazi kama mlinzi wa klabu ya usiku na kufanya kazi ya ufagiaji, kabla ya kuhitimu chuo kama mwanakemia.

Alifanya kazi katika kiwanda cha ndani na Esther Ballestrino, mwanaharakati aliyefanya kampeni dhidi ya udikteta wa kijeshi wa Argentina. Mwanamke huyo alitekwa, akapotea na hakupatikana tena.

Akawa Mjesuti, akasoma falsafa na kufundisha fasihi na saikolojia. Alitawazwa muongo mmoja baadaye, na kuwa mkuu wa mkoa wa kanisa hilo nchini Argentina 1973.

Jorge Mario Bergoglio alimrithi Papa Benedict

Jorge Mario Bergoglio alichaguliwa kuwa Papa na mkutano wa Makardinali mwaka 2013, baada ya mtangulizi wake, Papa Benedict, kujiuzulu. Alichaguwa jina lake la Papa katika kumuenzi Mtakatifu Francis wa Assisi, aliyekuwa mhubiri wa Karne ya 13 na mpenda wanyama. Jorge Mario Bergoglio, alikuwa Kardinali wa Argentina, na alikuwa na umri wa miaka sabini alipokuwa Papa mwaka 2013.

Mwaka 2013 Francis alikuwa Papa wa kwanza kutoka Amerika na kutoka Ulimwengu wa Kusini. Alimrithi Benedict XVI, ambaye alifariki mwaka 2022. Benedict XVI alikuwa Papa wa kwanza kustaafu kwa hiari baada ya takribani miaka 600.

Bergoglio aliwavutia wahafidhina juu ya mtazamo wake kwa masuala ya mahusiano, huku akiwavutia wanamageuzi kwa msimamo wake wa kiliberali juu ya haki za kijamii.

Ujumbe wa Amani

Alikuwa Askofu Msaidizi huko Buenos Aires mwaka 1992 na kisha akawa Askofu Mkuu.

Papa Yohane Paulo II alimteua kuwa kardinali mwaka 2001 na akachukua nyadhifa katika utumishi wa umma wa Kanisa.

Katika mahubiri yake, alitoa wito wa umoja katika jamii na kukosoa serikali ambazo zilishindwa kuwapa kipaumbele watu maskini zaidi katika jamii.

Akiwa Papa, alifanya juhudi kubwa kuponya mpasuko wa miaka elfu moja na Kanisa la Othodoksi la Mashariki.

Francis alifanya kazi na Waanglikana, Walutheri na Wamethodisti na kuwashawishi marais wa Israeli na Palestina kuungana naye kuombea amani.

Baada ya mashambulizi ya wapiganaji wa Kiislamu, alisema si sawa kuuhusisha Uislamu na vurugu.

Papa Francis alifanya mageuzi makubwa katika Kanisa Katoliki

Ndani ya urasimu wa Vatikani baadhi ya majaribio ya Francis ya kuleta mageuzi yalikumbana na upinzani, lakini alibaki kuwa maarufu miongoni mwa wanamapokeo.

Papa mpya aliweka misheni ya maadili kwa wafuasi bilioni 1.2 wa kanisa lake. “Oh, napendelea Kanisa maskini, na kwa watu maskini,” alisema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *