Mgombea urais Colombia ajeruhiwa kwa risasi

Kiongozi wa upinzani na mgombea urais nchini Colombia,Miguel Uribe, amepigwa risasi na kujeruhiwa wakati wa mkutano wa kampeni katika mji mkuu wa nchi hiyo, Bogota, siku ya Jumamosi(07.06.2025), taarifa hiyo ni kwa mujibu wa serikali.

Video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii inamuonyesha Miguel Uribe, mwenye umri wa miaka 39, akitoa hotuba mbele ya watu kadhaa wakati milio ya risasi ikisikika ghafla.

Katika picha nyingine, anaonekana akiwa amejiinamia kwenye gari, iliyotapakaa damu, huku kundi la watu kadhaa likijaribu kumnusuru. 

Meya wa Bogota,Carlos Fernando Galan, ameviambia vyombo vya habari kwamba kiongozi huyo amefanikiwa kufanyiwa upasuaji wa kwanza baada ya kufikishwa hospitalini akiwa katika hali mbaya.

Kijana wa miaka 15 anayedaiwa kumpiga risasi kiongozi huyo tayari amekamatwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *