Mgogoro Mashariki mwa DRC: Wakuu wa nchi wa SADC na EAC wateua wawezeshaji

Wakuu wa nchi za SADC na EAC wameteua wawezeshaji watatu wapya katika mgogoro wa mashariki mwa DRC, zaidi ya wiki mbili baada ya mkutano wao wa mwisho wa pamoja Februari 8 nchini Tanzania. Walikuwa wametoa wito wa “kusitisha mapigano mara moja na bila masharti” na “kusitishwa kwa uhasama” kati ya waasi wa AFC/M23 wanaoungwa mkono na jeshi la Rwanda na vikosi vya Kongo. Wito ambao haujatekelezwa. 

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Uteuzi huo unakuja wakati wakuu wa majeshi kutoka kambi hizo mbili za kikand walipokutana ili kutathmini njia ya kumaliza mgogoro huo.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari isiyo na tarehe, lakini iliyotolewa Februari 24, 2025, imefahamika kwamba Rais wa zamani wa Nigeria Olusegun Obasanjo, pamoja na Waziri Mkuu wa zamani wa Ethiopia, Hailemariam Desalegn watakuwa wawezeshaji wapya wa mchakato uliounganishwa wa Luanda na Nairobi, pamoja na Uhuru Kenyatta ambaye tayari alikuwa na wadhifa wa mwezeshaji wa mchakato wa Nairobi.

Kwa hiyo, Joao Lourenço, mwezeshaji wa mchakato wa Luanda, ambaye alikuwa ametangaza kwamba anajiuzulu kutoka wadhifa wake ili kuchukua nafasi ya mkuu wa Umoja wa Afrika, ameondoka. Kwa hivyo kazi ya viongozi hao watatu itakuwa kuratibu juhudi za kidiplomasia na usalama kwa nia ya kusitisha mapigano mashariki mwa DRC.

Kwa sababu sambamba na uteuzi huu, wakuu wa majeshi ktokaa kambi hizo mbili walikutana kwa mazungumzo, ili kujadili njia walizo nazo kutekeleza mahitimisho ya mkutano wa kilele wa Februari 8. Ijapokuwa hakuna taarifa yoyote iliyofichuliwa rasmi, ripoti iliyoshauriwa na Gazeti l Jeune Afrique inafahamisha kuwa muunganisho wa taratibu hizo mbili za amani uliwasilishwa na jopo la wataalamu kutoka EAC na SADC, hivyo kuwezesha mazungumzo kati ya pande zinazohusika katika mzozo huo ili kupelekea kusitishwa kwa uhasama.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa wakuu hao wa nchi, mkutano mpya utafanyika Februari 28 kujadili maelezo ya usitishaji mapigano.