Mgogoro Mashariki mwa DRC: Mwakilishi wa Marekani azuru Kinshasa kisha Kigali

Baada ya kuzuru Kinshasa, Mbunge wa Marekani Dk. Ronny Jackson ameendelea na ziara yake siku za hivi karibuni katika mji mkuu wa Rwanda Kigali, baada ya kutua huko Brazzaville. Dk. Ronny Jackson alikuwa daktari wa Rais Donald Trump wakati wa muhula wake wa kwanza na ni afisa mteule wa chama cha Republican kutoka jimbo la Texas. Suala la mzozo wa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) limekuwa kitovu cha ziara yake.

Imechapishwa:

Dakika 2

Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Kigali, Lucie Mouillaud

Wakati wa ziara yake ya siku mbili mjini Kigali, Mbunge kutoka chama cha Republican Dk. Ronny Jackson amekutana na Rais Paul Kagame kujadili “ushirikiano unaoendelea kukuza amani katika eneo hilo,” kulingana na ujumbe wa ofisi ya rais. Akiwa mkuu wa Kamati Ndogo ya Bunge ya Ujasusi na Operesheni Maalum, daktari huyo wa zamani wa Ikulu ya Marekani na Admirali aliyestaafu katika jeshi la majini pia amekutana na watu wawili kutoka vyombo vya usalama vya Rwanda: Waziri wa Ulinzi Juvénal Marizamunda na Katibu Mkuu wa Ujasusi Aimable Havugiyaremye.

Ziara hiyo inajiri siku chache baada ya kufanya ziara mjini Kinshasa, ambako mzozo wa mashariki mwa DRC ulikuwa kiini cha mijadala. Ronny Jackson alikutana na viongozi wa kidini na pia Mkuu wa Nchi Félix Tshisekedi, ambapo alisema kuwa anataka kufanya kazi ili kurejesha amani nchini, kwa mujibu wa ofisi ya rais, na kwamba makampuni ya Marekani yanaweza kuja kuwekeza nchini DRC.

Ujumbe uliotolewa wakati ushirikiano wa uchimbaji madini kwa sasa unajadiliwa na Marekani.

Wengi wa watu 100,000 waliokimbia makazi yao nchini Uganda na Burundi wanajikuta katika “hali mbaya”

Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, zaidi ya watu 100,000 waliokimbia vita mashariki mwa DRC wamepata hifadhi katika muda wa chini ya miezi mitatu katika nchi jirani za Uganda na Burundi. Mapigano katika mikoa ya Kivu Kaskazini na Kivu Kusini yamewalazimu watu  kutoroka makazi yao. Lakini hali yao inaleta matatizo mengi katika nchi zinazowapokea, kama ilivyoelezwa na msemaji wa UNHCR mjini Geneva, Eujin Byun.

Hali katika nchi jirani ni mbaya, kwanza kwa sababu nchi hizi mbili tayari zimepokea mamilioni ya wakimbizi. Kwa hiyo tunaweza kuona mzigo mzito walio nao katika kuwahifadhi na kuwakaokea wakimbizi hawa. Hata hivyo, kutokana na ukosefu wa fedha wa hivi majuzi na uhaba wa fedha, hatuwezi kukabiliana mara moja na dharura hii. Hii ina maana kwamba idadi kubwa ya wakimbizi wanaowasili kutokana na mzozo nchini DRC wanajikuta katika hali ya msongamano mkubwa wa maisha, na ukosefu wa huduma za msingi kama vile maji, chakula na malazi. Aidha, kwa sasa tumebaini wagonjwa wanane wa kipindupindu, jambo linaloonyesha kuwa mfumo wa afya hautoshi katika nchi hizi mbili, hivyo kuongeza hatari ya kuenea kwa magonjwa mengine.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *