Mgogoro mashariki mwa DRC katika ajenda ya mkutano usio wa kawaida wa SADC

Mkutano usio wa kawaida wa viongozi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) utafanyika kwa njia ya video leo Alhamisi, Machi 13. Mkutano huo ukiongozwa na Emmerson Mnangagwa, rais wa Zimbabwe, utajaribu kufafanua hatma ya jeshi lililotumwa na jumiya hiyo mashariki mwa DRC, eneo ambalo linakabiliwa na mzozo mkali.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu mjini Kinshasa, Paulina Zidi

Mkutano huo usio wa kawaida wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), ambao umepangwa kufanyika Alhamisi hii, Machi 13, kwa njia ya video, unafuatia mkutano wa troika ya jumuiya ya kikanda – muundo wa SADC unaoangazia masuala ya kisiasa, ulinzi na usalama – Machi 6, ambapo mfululizo wa mapendekezo yalitolewa ambayo lazima sasa yaidhinishwe na wakuu wa nchi.

Miongoni mwa masuala makuu yatakayoamuliwa: mustakabali wa kikosi cha kijeshi kilichotumwa nchini, SAMIDRC, ambacho kilikuwa kimeundwa kuchukua nafasi ya kikosi cha jumuiya nyingine ya kikanda, Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), ambacho Kinshasa ilitaka kiondoke mara moja katika ardhi ya DRC. Tangu kutekwa kwa Goma na kundi la waasi la AFC/M23 mwishoni mwa mwezi wa Januari, wanajeshi wa SADC wamekuwa wakisubiri ufafanuzi wa hali yao. “Kikosi hiki sasa kimezingirwa na Rwanda,” “kikosi hiki kiaonekana kuelekea kujiondoa taratibu,” kinabainisha chanzo cha Kongo kilicho karibu na suala hilo.

Swali linabaki: ikiwa kikosi hiki kitaondoka , ni kikosi gani kinachoweza kuchukua nafasi yake? Wakati mchambuzi mmoja anabaini kwamba “wazo la kikosi kisichoegemea linaonekana kusahaulika,” jibu linaweza kutoka katika mkutano ambao umesubiriwa kwa wiki kadhaa, ambao utawakutanisha wakuu wa diplomasia wa SADC na EAC. Mkutano ambao unaweza kufanyika wiki ijayo…

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *