Mfahamu mtu aliyeshinda Grammy nyingi lakini hajawahi kuimba kwenye maisha yake

Marekani. Quincy Jones hajawahi kuimba kwenye maisha yake lakini kawazidi wasanii wengi maarufu kwenye orodha ya Grammy kama vile Rihanna, Taylor Swift, Michael Jackson, na Lady Gaga. 

Wakati Beyonce akiwa ndiye kinara kwa wasanii wenye tuzo nyingi za Grammy duniani akiwa ameshinda mara 32, kuna huyu mtayarishaji nguli wa muziki duniani Quincy Jones ambaye ana tuzo 28 za Grammy huku akiwa amechaguliwa kuwania mara 80.

                      

Ushindi huo wa Tuzo za Grammy unamweka juu zaidi ya wasanii kama Jay Z na YE, Kanye West wakiwa na tuzo 24, Adele akiwa na tuzo 16, Eminem mwenye tuzo 15, Taylor Swift mwenye tuzo 14, Michael Jackson, Lady Gaga wakiwa na tuzo 13 kila mmoja, na Rihanna mwenye tuzo 9 za Grammy 

Wasanii pekee wanaomshinda Jones tuzo za Grammy ni Beyonce mwenye tuzo 32 na George Solt mwenye tuzo 31 

Quincy Jones alizaliwa 1933 huko Chicago ni mtayarishaji wa muziki yaani Producer, miaka ya 1950 kabla hajaanza kutayarisha kazi za wasanii wengine aliwahi kufanya kazi na mwanamuziki Frank Sitara, lakini anakumbukwa zaidi kwa kutayarisha albamu 3 za Michael Jackson zilizofanya vizuri sokoni ambazo ni ‘Off The Wall, Thriller, na Bad, Jones.

Alianza kutayarisha muziki wa jazi miaka ya 1970 kabla hajahamia kwenye muziki wa Pop, Huku Grammy nyingi alizowania na kushinda kwa miaka yote ni kutokana kazi alizotayarisha kwa wasanii. 

Jones akiwa na miaka 86, alifanya kazi na wasanii wa kizazi kipya ambapo alionekana kwenye video Travis Scott na young Thug ya mwaka 2020. Quincy Jones alifariki mapema mwezi huu, Novemba 3 2024 akiwa na umri wa miaka 91