#MEZAHURU: Maegesho ya magari na Malipo. Tunangali juu ya maegesho ya magari na namna ya kulipa madeni ya maegesho hayo. Kumekuwa na kero kubwa kwa watumia vyombo vya moto na malipo ya madeni ya maegesho hayo. Wengine wanaegesho nje ya maeneo ya makazi yao na kuandikiwa malipo. Je, ni sahihi na unalipa kodi ya ardhi? wengine gari imesafiri au haijatoka au iko gereji huku inakuja taarifa ya kudaiwa. Wengine wanaandikiwa malipo ya maeneo ambayo hata hajawahi kufika kabisa, ukiuliza majibu ni kwamba lazima ulipe ndio upeleke malalamiko ofisini kwao.