Mexico yatangaza kuwarejesha nchini Marekani walanguzi 29 wa dawa za kulevya

Mexico imewatuma Marekani watu 29 kati ya wafanyabiasahra wake hatari zaidi wa dawa za kulevya waliokuwa wanafungwa. Njia mpya ya kumfurahisha Donald Trump wakati rais huyo wa Marekani alithibitisha utumiaji wa ushuru wa forodha kwa bidhaa zinazotoka Mexico kuanzia Machi 4. Miongoni mwa wahalifu hawa kuna viongozi wa uhalifu uliopangwa nchini Mexico.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu huko Mexico, Marine Lebègue

Mexico imetangaza Alhamisi, Februari 27, kusafirishwa kwa walanguzi 29 wa dawa za kulevya nchini Marekani. Mamlaka ya Mexico imetangaza kusafirishwa kwa fanyabiashara wa dawa za kulevya kutoka kundi hili la kipekee mapema alasiri hii, wakati sehemu kubwa ya serikali iko Washington ili kuzuia serikali ya Donald Trump kutoza ushuru wa 25% kwa mauzo yake kuanzia siku ya Jumanne, Machi 4.

Caro Quintero, the Zetas, el Guerito… majina haya yanajulikana kwa watu wote wa Mexico. Viongozi wa makundi haya, wauaji waliohusika na visa mbalimbali vya mauaji, kwa miaka mingi waliitisha nchi, kabla ya kukamatwa na kufungwa huko Mexico. Miongoni mwa viongozi hao wa uhalifu ni ndugu wawili, waliopewa majina ya utambulisho kwa ajili ya usalama wao ya Z-40 na Z-42, wanajeshi wa zamani katika jeshi la Mexico ambao walikuja kuwa washirika muhimu wa kundi la Golfo, ambalo linaendesha harakati zake kaskazini mwa Mexico.

Mhalifu aliyetafutwa kwa muda mrefu

Lakini mhalifu mkuu ambaye Marekani ilikuwa ikimsubiri zaidi ni Rafael Caro Quintero. Mwanzilishi wa kundi la Guadalajara na kiongozi wa kihistoria wa wafanyabiashara wa dawa za kulevya nchini Mexico, anayechukuliwa kuwa adui wa umma nambari 1 na shirika la Marekani linalopambana dhidi ya usafirishaji wa dawa za kulevya, anasemekana kuwateka nyara, kuwatesa na kuwaua maafisa wake wawili.

Amehamishiwa Marekani, pamoja na wafungwa wengine 28, na kuifanya kuwa uhamisho mkubwa zaidi kuwahi kufanywa na Mexico nchini Marekani. Walipofikishwa nchini Marekani wamejiunga na walanguzi mashuhuri wa dawa za kulevya kama vile El Chapo Guzman na El Mayo Zambada, wote waanzilishi wa kundi maarufu la Sinaloa.