
Takriban watu 32 wamefariki siku ya Jumatatu Machi 10 katika ajali mbili za basi huko Mexico, viongozi wa majimbo ya Oaxaca (kusini) na Durango (kaskazini) wamesema.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Takriban watu 18 wamefariki wakati basi lilipopinduka kwenye barabara kuu katika jimbo la Oaxaca, serikali ya eneo hilo imesema. Mamlaka iliripoti idadi ya vifo vya watu kumi na moja mapema Jumatatu. Takriban watu kumi bado wamelazwa hospitalini, kulingana na chanzo hicho. Kwa mujibu wa vyombo kadhaa vya habari vya Mexico, wahanga walikuwa wafuasi wa chama tawala cha mrengo wa kushoto ambao walikuwa wakirejea kutoka kwenye mkutano mkubwa uliofanyika siku ya Jumapili huko Mexico ambao Rais Claudia Sheinbaum alishiriki, kupinga vitisho vya forodha vya Rais wa Marekani Donald Trump. Mamlaka za eneo hilo “zitafanya uchunguzi unaohitajika ili kubaini sababu za ajali,” wametangaza katika taarifa. Basi hilo lilipinduka karibu na Santo Domingo Narro, kusini-kati mwa jimbo la Oaxaca, ambalo mji mkuu wake wa jina moja na pwani ya Pasifiki ni maarufu kwa watalii.
Siku hiyo, takriban watu 14 walifariki katika baada ya lori na basi kutoka Marekani kugongana, kikosi jamii katika jimbo la Durango kimesema. Abiria kumi walinusurika. Basi hilo lilikuwa limeondoka McAllen kwenye mpaka wa Texas na Mexico, ambako watu wengi wa Mexico wanafanya kazi. Gari hilo lilishika moto, kulingana na video kwenye mitandao ya kijamii. Chanzo cha ajali hakijabainishwa.