
Ndege za kijasusi za Marekani zimeruka kwenye anga ya Mexico. Katika wiki mbili zilizopita, misheni kadhaa za uchunguzi zimeripotiwa kufanywa na jeshi la Marekani kwenye mipaka ya Mexico. Ingawa serikali ya Mexico inadai kutojua lengo la misheni hizi, kila kitu kinaonyesha kuwa ni sehemu ya vita vya Donald Trump dhidi ya magenge ya wafayabiashara haramu.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Jeshi la Marekani limeongeza kwa kasi ufuatiliaji wake wa magenge ya wafanyabiashara haramu wa Mexico katika wiki mbili zilizopita, na ndege za kijasusi za kisasa zikifanya angalau misheni 18 zikiruka anga ya kusini magharibi mwa Marekani na katika anga ya kimataifa karibu na rasi ya Baja California, kulingana na data ya open source na maafisa watatu wa Marekani wanaofahamu misheni hiyo, CNN imeripoti. Hii haijawahi kushuhudiwa hapo awali. Hatimaye serikali ya Mexico imekiri kuona ndege mbili kati ya hizi, lakini bila kujua dhamira yao, anaripoti mwandishi wetu huko Mexico, Marine Lebegue.
Bila kuingia katika anga ya Mexico, ndege hizi za Marekani zilizobobea katika ujasusi ziliruka karibu sana na mpaka wa kaskazini na pwani ya magharibi ya Mexico, nje ya pwani ya Sinaloa, eneo linalodhibitiwa na genge lenye nguvu la wafanyabiasahara wa madawa ya kulevya la Sinaloa, kwa muda wa siku kumi.
Donald Trump ametangaza vita dhidi ya magenge ya wafanyabiashaharamu ya madawa ya kulevya kutoka Mexico
Mara tu alipoingia madarakani, Donald Trump alitangaza vita dhidi ya magenge hayo kutoka Mexico, ambayo anashutumu kuhusika na biashara haramu ya fentanyl, dawa ambayo inaangamiza Marekani. Wiki mbili zilizopita Rais wa Mexico Claudia Sheinbaum alikubali kutuma wanajeshi 10,000 kwenye mpaka wa nchi hizo mbili ili kuzuia fentanyl kuingia Marekani. Kutumwa huku kulikubaliwa na Donald Trump badala ya kusitishwa kwa mwezi mmoja kwa ushuru wa forodha ambao rais wa Marekani anataka kulazimisha kwa Mexico, hali ambayo inaweza kudhoofisha uchumi wa nchi hiyo.