Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, Meja Jenerali Rajabu Mabele akizungumza wakati wa hafla ya kuhitimisha Mafunzo ya Vijana wa Kujitolea OP Miaka 60 ya Muungano Ruvu JKT katika kambi ya RUVU JKT 832 KJ iliyopo Mlandizi mkoani Pwani. Hafla hiyo imefanyika Aprili 17, 2025.
NA EMMANUEL MBATILO, PWANI
MKUU wa Jeshi la Kujenga Taifa, Meja Jenerali Rajabu Mabele amewataka wahitimu wa mafunzo ya kijeshi kutunza afya zao kwani wakiwa na afya njema watapata fursa nyingi zilizopo nchini ikiwemo kupata nafasi katika kada mbalimbali za ulinzi.
Amewaagiza wahitimu hao kujiepusha na matumizi ya vileo mbalimbali ikiwemo matumizi ya dawa za kulevya kwani si sehemu ya maadili ya mafunzo ya kijeshi.
Tamko hilo amelitoa Aprili 17,2025 katika Kambi ya RUVU JKT 832 KJ alipokuwa akihitimisha Ufungaji wa Mafunzo ya Vijana wa Kujitolea OP Miaka 60 ya Muungano Ruvu JKT.
Amesema madhumuni ya mafunzo hayo ni kulea vijana wakitanzania katika maadili na kushiriki katika mafunzo ya ulinzi wa nchi pamoja na kukuza moyo wa kizalendo.
“Malengo makuu kwenye mafunzo haya ni pamoja na kuhakikisha vijana wanasifa nne kuu za msingi ambazo ni nidhamu, uaminifu, utiifu kwa viongozi na nchi yao, lakini pia kuwafanya kuwa hodari katika kazi, hali ambayo vijana hawa ambao wamehitimu wanayo”. Amesema Meja Jenerali Mabele.
Kwa upande wake, Brigedia Jenarali Aboubakar Charo, ambaye alimwakilisha Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi amesema amethibitisha kuwa vijana hao wamepokea mafunzo hayo na wameiva kwani wamekuwa na ukakamavu, uzalendo, uhodari, uvumilivu na kujiamini.
Aidha Jenerali Charo amewataka vijana hao kuwa tayari kwaajili ya mafunzo ya stadi za kazi na maisha katika kipindi cha miezi 20 ijayo.
Hata hivyo Jenerali Charo amewakumbusha wahitimu hao kukumbuka falsafa ya kazi iendelee ikiwa ni kuunga juhudi za Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuleta Maendeleo ya nchi.
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, Meja Jenerali Rajabu Mabele akikagua gwaride wakati wa hafla ya kuhitimisha Mafunzo ya Vijana wa Kujitolea OP Miaka 60 ya Muungano Ruvu JKT katika kambi ya RUVU JKT 832 KJ iliyopo Mlandizi mkoani Pwani. Hafla hiyo imefanyika Aprili 17, 2025.
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, Meja Jenerali Rajabu Mabele akizungumza wakati wa hafla ya kuhitimisha Mafunzo ya Vijana wa Kujitolea OP Miaka 60 ya Muungano Ruvu JKT katika kambi ya RUVU JKT 832 KJ iliyopo Mlandizi mkoani Pwani. Hafla hiyo imefanyika Aprili 17, 2025.
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, Meja Jenerali Rajabu Mabele akizungumza wakati wa hafla ya kuhitimisha Mafunzo ya Vijana wa Kujitolea OP Miaka 60 ya Muungano Ruvu JKT katika kambi ya RUVU JKT 832 KJ iliyopo Mlandizi mkoani Pwani. Hafla hiyo imefanyika Aprili 17, 2025.
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, Meja Jenerali Rajabu Mabele akizungumza wakati wa hafla ya kuhitimisha Mafunzo ya Vijana wa Kujitolea OP Miaka 60 ya Muungano Ruvu JKT katika kambi ya RUVU JKT 832 KJ iliyopo Mlandizi mkoani Pwani. Hafla hiyo imefanyika Aprili 17, 2025.
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, Meja Jenerali Rajabu Mabele akizungumza wakati wa hafla ya kuhitimisha Mafunzo ya Vijana wa Kujitolea OP Miaka 60 ya Muungano Ruvu JKT katika kambi ya RUVU JKT 832 KJ iliyopo Mlandizi mkoani Pwani. Hafla hiyo imefanyika Aprili 17, 2025.
Mwakilishi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Brigedia Jenarali Aboubakar Charo akizungumza wakati wa hafla ya kuhitimisha Mafunzo ya Vijana wa Kujitolea OP Miaka 60 ya Muungano Ruvu JKT katika kambi ya RUVU JKT 832 KJ iliyopo Mlandizi mkoani Pwani. Hafla hiyo imefanyika Aprili 17, 2025.
Mkuu wa Tawi la Mafunzo JKT- Kanali Longinus Nyingo akizungumza wakati wa hafla ya kuhitimisha Mafunzo ya Vijana wa Kujitolea OP Miaka 60 ya Muungano Ruvu JKT katika kambi ya RUVU JKT 832 KJ iliyopo Mlandizi mkoani Pwani. Hafla hiyo imefanyika Aprili 17, 2025.
Kamanda wa Kikosi Ruvu JKT, Peter Mnyani akizungumza wakati wa hafla ya kuhitimisha Mafunzo ya Vijana wa Kujitolea OP Miaka 60 ya Muungano Ruvu JKT katika kambi ya RUVU JKT 832 KJ iliyopo Mlandizi mkoani Pwani. Hafla hiyo imefanyika Aprili 17, 2025.

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, Meja Jenerali Rajabu Mabele akitoa zawadi kwa wahitimu wa Mafunzo ya Vijana wa Kujitolea OP Miaka 60 ya Muungano Ruvu JKT waliofanya vizuri katika kambi ya RUVU JKT 832 KJ iliyopo Mlandizi mkoani Pwani. Hafla hiyo imefanyika Aprili 17, 2025.

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, Meja Jenerali Rajabu Mabele akifurahi na wahitimu wa Mafunzo ya Vijana wa Kujitolea OP Miaka 60 ya Muungano Ruvu JKT katika kambi ya RUVU JKT 832 KJ wakati wa hafla ya kuhitimisha Mafunzo hayo Aprili 17, 2025 Mlandizi mkoani Pwani.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
The post MEJA JENERALI MABELE: MAFUNZO YA JKT YANALENGA KUKUZA UZALENDO NA MAADILI appeared first on Mzalendo.
Post Views: 6