Mchongo wa Nandy kusainiwa WCB ulikwama hivi

Dar es Salaam. Mwanamuziki Nandy amesema kabla ya kujiunga na ‘Tanzania House of Talents’ (THT) alitaka kujiunga na rekodi lebo ya WCB iliyopo chini ya Diamond.

Nandy ambaye ni mmiliki wa rekodi lebo ya African Princess, inayomsimamia mwanamuziki Yammy, wakati akifanya mahojiano na Crown Media amesema ndoto yake hiyo ilibadilika baada kurudi kutoka kwenye shindano ya ‘Tecno Own The Stage 2025’ ambalo aliibuka mshindi 

                       

New Content Item (1)
New Content Item (1)

” Kabla ya kwenda Tecno Own The Stage nilikutana na Diamond na Babu Tale tukakubaliana nikirudi nianze WCB. Nakumbuka nimerudi kutoka Tekno nikijua kama nimeshinda nikienda kwa wadau mambo yote yatakuwa mazuri. 

“Nilivyorudi nilikutana na watu tofauti tofauti wakanishauri niende THT kwa ajili ya kujifunza zaidi. Kipindi hicho hata wao (Diamond) walikuwa wanafanya kazi na Boss Ruge nikaona sawa,”amesema. 

                     

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Utakumbuka kuwa Nandy katika mashindano hayo alikuwa mshindi wa pili na kuondoka na kitita cha $15,000 Sh milioni 36. Pia alipata nafasi ya kupikwa kimuziki chini ya label ya Chocolate City ambayo imekuza majina ya wasanii kama M.I., Ice Prince, Victoria Kimani na wengine.