Mchambuzi Mzayuni: Israel imepigishwa magoti na kusalimu amri mbele ya mkakati wa Hamas

Mwandishi mmoja wa Israel amesema katika uchambuzi wake kwamba, tofauti kati ya matukio ya miinuko ya Jabal al-Sheikh huko Syria na yale ya Ghaza ni kwamba, kinyume na ilivyokuwa kwa jeshi la Syria, Hamas wao walikuwa wamejitayarisha na kujipanga vizuri na kupata turufu kwa kuwateka wakazi wengi wa utawala wa Kizayuni.