Mbunge wa Singida Kaskazini, Abeid Ramadhani, amesema kuwa kwa kuzingatia hatua kubwa ambazo serikali imepiga katika uboreshaji …

Mbunge wa Singida Kaskazini, Abeid Ramadhani, amesema kuwa kwa kuzingatia hatua kubwa ambazo serikali imepiga katika uboreshaji …

Mbunge wa Singida Kaskazini, Abeid Ramadhani, amesema kuwa kwa kuzingatia hatua kubwa ambazo serikali imepiga katika uboreshaji wa miundombinu, sasa ni wakati muafaka kwa serikali kuelekeza nguvu zake kwenye ujenzi wa uchumi wa viwanda.

Amesema kuwa miundombinu bora ni msingi muhimu wa maendeleo ya viwanda, hivyo hatua inayofuata ni kutumia fursa hiyo kuwawezesha Watanzania kiuchumi.

Akizungumza wakati wa mahojiano maalum na UTV kuelekea kusomwa kwa Bajeti Kuu ya Serikali, Ramadhan alisisitiza kuwa mkazo zaidi unatakiwa kwenye sekta ya viwanda kwa kuwa ndiyo njia ya kuongeza thamani ya mazao ya kilimo, kutoa ajira na kukuza pato la mtu mmoja mmoja pamoja na taifa kwa ujumla.

#AzamTVUpdates
✍Juliana James
Mhariri | John Mbalamwezi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *