Mbunge wa Mbulu, Flatei Massay amesema kuwa bajeti ya mwaka huu ikijielekeza kwenye sekta ya kilimo, itachangia kwa kiasi kikubw…

Mbunge wa Mbulu, Flatei Massay amesema kuwa bajeti ya mwaka huu ikijielekeza kwenye sekta ya kilimo, itachangia kwa kiasi kikubw…

Mbunge wa Mbulu, Flatei Massay amesema kuwa bajeti ya mwaka huu ikijielekeza kwenye sekta ya kilimo, itachangia kwa kiasi kikubwa kuinua uchumi wa taifa pamoja na maisha ya wananchi mmoja mmoja.

Akizungumza katika kipindi maalum cha UTV kuelekea kusomwa kwa Bajeti Kuu ya Serikali, Massay ameeleza kuwa kilimo kina nafasi muhimu katika maendeleo ya nchi, hivyo serikali inapaswa kukipa kipaumbele kikubwa.

Ameishauri serikali kuwekeza zaidi katika utoaji wa ruzuku kwa mbegu bora na pembejeo za kilimo, sambamba na kuboresha miundombinu ya skimu za umwagiliaji ili kuhakikisha wakulima wanalima kwa uhakika katika kipindi chote cha mwaka.

#AzamTVUpdates
✍Juliana James
Mhariri | John Mbalamwezi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *