Mbunge wa Kinondoni, Abbas Tarimba, amependekeza kuwa miongoni mwa vipaumbele vya bajeti ya mwaka huu iwe ni kukamilisha miradi …

Mbunge wa Kinondoni, Abbas Tarimba, amependekeza kuwa miongoni mwa vipaumbele vya bajeti ya mwaka huu iwe ni kukamilisha miradi …

Mbunge wa Kinondoni, Abbas Tarimba, amependekeza kuwa miongoni mwa vipaumbele vya bajeti ya mwaka huu iwe ni kukamilisha miradi ya kimkakati iliyoanzishwa, ili wananchi waanze kunufaika na matokeo ya miradi hiyo.

Amesema kuwa miradi hiyo inalenga kuboresha maisha ya wananchi na kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi, hivyo kukamilika kwake ni muhimu kwa ustawi wa taifa.

Akizungumza na UTV katika kipindi maalum kuelekea kusomwa kwa Bajeti Kuu ya Serikali, Tarimba ameeleza kuwa kukamilika kwa miradi hiyo kutaleta tija kwa wananchi na pia kuipunguzia serikali hasara inayotokana na ucheleweshaji wa utekelezaji wake.

#AzamTVUpdates
✍Alpha Jenipher
Mhariri | John Mbalamwezi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *