Mbunge wa Busanda alia ukubwa wa Jimbo aomba ligawanywe

Geita. Mbunge wa Busanda Tumaini Magesa amekiomba kikao cha Kamati cha Ushauri wa Mkoa (RCC) kuziagiza mamlaka za chini kuharakisha mchakato w amaombi wa kugawa jimbo la Busanda ili ywe majimbo mawili kutokana na ukubwa wake.

Magesa amesema jimbo la Busanda ni la nne kwa ukubwa nchini likiwa na kata 22 na tarafa mbili hivyo ni vema likagawanywa mara mbili ili wnanachi wake waweze kupata huduma zinazostahili kwa wakati.

“Mwenyekiti Tume Huru ya Uchaguzi ilitangaza toka februari 26 kuwa yapelekwe mapendekezo ya ukataji wa majimbo ya uchaguzi na kw awale wanaotaka kubadilisha majina,Busanda kwenye rekodi za serikali ni jimbo la nne kwa ukubwamimi naomba mamlaka za chini ziharakishwe ili mchakato huu ufanyike mapema,amesema Magesa.

Amesema ukubw awa jimbo hilo husababisha wananchi kutofikiwa na huduma ipasavyo akitolea mfano Serikali inaposema kila jimbo litapewa Sh500 kwa ajili ya matengenezo ya barabara inakuwa ngumu kuhudumia kata 22 wakati Mbunge mwingine anahudumia kata nane au tisa.

“Mfano Bungeni wanasema kila jimbo itapata kituo cha afya au shule mimi nina kata 22 nagaiwa sawa na yule mwenye kata 8 kwa ukubwa wa jimbo hili na wingi wa watu napendekeza kikao hiki kiagize mamlaka za chini kutekeleza mchakato mapema ili tarafa mbili za Busanda na Butundwe zikatwe majimbo mawiliamesema Magesa

Magesa amesema Kata za Butundwe na Busanda zinakidhi vigezo kwakuwa zote zina wananchi zaidi ya 400,000 huku Butundwe kiuchumi ikibebwa na Mji mdogo wa Katoro na Busanda ikibebwa na uchimbaji wa dhahabu ulioshamiri kwenye kata za Nyarugusu na Rwamgasa.

Mkuu wa Mkoa wa Geita ambae ni mwneyekiti wa kiako hicho amepokea hoja ya Magesa na kuagiza katibu tawala mkoa kuziandikia mamlaka zinazohusika ili zikamilishe mchakato haraka waweze kupeleka mapendekezo kwenye Tume huru ya Uchaguzi

Ameagiza vikao vya mabaraza ya madiwani na kikao cha ushauri cha wilaya kupitisha ajenda hiyo kabla ya Machi 14,2025 ili mkoa ufanye kikao maalum cha Ushauri cha Mkoa Machi 14 kupitisha mapendekezo ya ya majimbo yaliyoomba kugawanywa

“ Tufanye RCC maalum kwa ajili ya kupitisha mapendekezo na maombi ya maeneo yanayoomba kugawanywa kwenye majimbo,najua kugawa majimbo kunaweza kugusa kata kwa zile kata zitakazoguswa basi ni vema mmpendekeze hizo pia”

Amesema tayari Wilaya ya Chato wamekaa kiako cha baraza cha kugawa jimbo na sasa inasubiriwa DCC na kuagiza wakamilishe mchakato huo haraka kabla ya Machi 14,ili Mkoa uweze kupitisha na kuwasilisha kwenye Tume huru ya Uchaguzi ambayo ndio yenye mamlaka ya kuridhia au kupinga.

Baadhi ya wananchi wamesema kugawanywa kwa majimbo kutasaidia huduma kusogezwa karibu na kwa haraka tofauti na ilivyo sasa.

Ikorongo Otto mkazi wa Geita amesema jimbo ni uwakilishi wa wananchi kwenye mgawanyo wa keki ya Taifa na linapokuwa kubwa na mwakilishi mmoja uwakilishi unakuwa mdogo kwa wannachi.

“Ni afandhali maeneo yatengenezwe mengi ili wananchi wa eneo husika waweze kunufaika na keki ya Taifa nimpongeze Mbunge kwa kuona haja ya kupatikana kwa jimbo la Butundwe ili wananchi wafikiwe na huduma wannachi hawaamini kama madiwani ni wawakilishi wao ndio maana unaona wanaolalamikiwa ni wabunge na sio madiwani,”amesema Otto

Mkoa wa Geita una majimbo saba ambayo ni Geita Mji,Geita,Busanda,Chato,Nyang’hwale,Mbogwe na Bukombe.

Tayari Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imetangaza kuanza mchakato wa kuchunguza,kugawa au kubadili majina ya majimbo ya uchaguzi kwa mujibu wa kanuni ya 18(1) ya kanuni ya Tume huru ya Uchaguzi za mwaka 2024 na mapendekezo yatapokelewa kuanzia Februari 27 hadi machi26,2025