Mbunge wa Bunge la Ulaya: Marekani na waitifaki wake wanaendesha vita Ukraine kwa ajili ya viwanda vyao vya kijeshi

Pars Today: Mbunge wa Ireland katika Bunge la Ulaya amesema kuwa, madola ya Ulaya na Marekani wamelipa uhai mpya shirika la kigaidi liitwalo NATO kupitia vita vya Ukraine.

Michael Wallace, mbunge wa Ireland katika Bunge la Ulaya amelishambulia vikali shirika la kijeshi la nchi za Magharibi NATO.

Kwa mujibu wa Pars Today, mbunge huyo ameandika katika mtandao wa kijamii wa X kwamba, Ulaya na Marekani hawataki kupatikane suluhu na amani huko Ukraine. Wanataka kulipa uhai mpya shirika la kigaidi linalitwa NATO. Wanataka kuchuma faida kubwa kwa ajili ya viwanda vyao vya kijeshi na hakuna sehemu bora ya kufanyia hilo isipokuwa ni Ukraine.

Vita nchini Ukraine vilianza tarehe 24 Februari 2022 na vinaendelea hadi hivi sasa. Vita hivyo vilichochewa na madola ya Magharibi ambayo yaliisukuma ukutani Russia mpaka ikashindwa kuvumilia tena na kuamua kulinda usalama na maslahi yake ya kitaifa katika mipaka yake kwa kuingia vitani na Ukraine.