
Mbunge wa upinzani nchini Senegal ambaye ni mshirika wa karibu wa rais wa zamani wa nchi hiyo Macky Sall ameshtakiwa na kufungwa jela huko Dakar siku ya Alhamisi kwa “utakatishaji fedha, ulaghai wa fedha za umma na njama za uhalifu”, mmoja wa mawakili wake ameliambia shirika la habari al AFP, akisema “ameshangazwa” na uamuzi huo.
Imechapishwa:
Dakika 2
Matangazo ya kibiashara
Mouhamadou Ngom, anayejulikana kama Farba, pia meya wa wilaya ya kaskazini mwa nchi, amesikilizwa na jaji kutoka kitengo cha mahakama ya kifedha (PJF), chombo cha kupambana na rushwa, kilichomfunga, amesema mmoja wa wanasheria wake Doudou Ndoye. “Aliwekwa chini ya waranti kwa mshangao mkubwa wa mawakili wake ambao wameshangazwa na utaratibu ambao haulingani na sheria zozote za sheria za Senegal. Mtuhmiwa huyo hasemi chochote kuhusu alichokifanya. Anawekwa gerezani akisubiri kujua alichokifanya,” ameongeza wakili Ndoye.
Bunge la Senegal, ambalo liliombwa na PJF, chombo kilichoundwa na mamlaka ya zamani, mnamo Januari 24 iliondoa kinga ya ubunge ya Bw. Ngom ili aweze kusikilizwa na mahakama kufuatia tuhuma za kuhusika kwake katika makosa. Upande wa ofisi ya mashitaka wa mahakama hii ulidai kupokea taarifa kutoka kwa Kitengo cha Taifa cha Usindikaji Taarifa za Fedha (Centif), ambacho ni chombo cha Wizara ya Fedha, ambacho kiliwasilisha kwa taasisi ya Bunge, inayodhibitiwa kwa kiasi kikubwa na serikali, kwa ajili ya kuondoa kinga ya Bw. Ngom, mtu wa kutumainiwa wa aliyekuwa Rais Sall (2012-2024).
“Uchunguzi uliofanywa unaonyesha mbinu za kisasa za utakatishaji fedha kupitia makampuni ya makubwa ambayo yalidaiwa kutumika kwa shughuli za kutiliwa shaka zenye thamani ya muda iliyokadiriwa kuwa ya zaidi ya faranga za CFA bilioni 125” (zaidi ya euro milioni 192), ofisi ya mwendesha mashtaka wa PJF ilisema katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyochapishwa Januari 12. Watu wengine kadhaa walio karibu na serikali ya zamani wametajwa katika kesi hii, kulingana na vyombo vya habari vya ndani. Makumi ya wafuasi wa Mbunge Ngom walioandamana siku ya Alhamisi karibu na makao makuu ya PJF, mkabala na Chuo Kikuu cha Dakar, walitawanywa na polisi, mpiga picha wa shirika la habari la AFP amebainisha.
Kwa wiki kadhaa,wasaidizi wa mbunge huyo wamekuwa wakilaani mauaji kwa “utaratibu wa kisiasa” na mahakama. Serikali mpya ya Senegal, iliyotokana na uchaguzi wa mwezi Machi wa Rais Bassirou Diomaye Faye, imeahidi kuvunja mfumo wa zamani. Mnamo mwezi Septemba, Waziri Mkuu Ousmane Sonko aliahidi uchunguzi kuhusu “ufisadi ulioenea” ambao alisema ulikuwa umeenea chini ya utawala wa zamani. Maafisa kadhaa wa zamani wameshtakiwa na kufungwa jela katika miezi ya hivi karibuni.