Mbappe alivyopishana na Samatta Taifa Stars

Mara ya mwisho kwa John anayechezea Aalborg ya Denmark kujumuishwa katika kikosi cha Taifa Stars ilikuwa ni Juni 11, 2024 wakati timu hiyo ilipokabiliana na Zambia katika mashindano hayo ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia ambapo timu hiyo iliibuka na ushindi wa bao 1-0 ugenini huko Zambia.

Hata hivyo mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 21, hatocheza sambamba na nahodha wa timu hiyo, Mbwana Samatta anayechezea PAOK ya Ugiriki ambaye hajajumuishwa kikosini kutokana na majeraha.

“Samatta ni majeruhi na ana wiki mbili hadi tatu kuwa sawa. Aliumia mazoezini na baada ya kupata ile taarifa tulishtuka lakini baadaye tulijiridhisha. Mchango wa Samatta tulikuwa tunaihitaji kuliko wakati wowote ukilinganisha na kiwango chake.

“Lakini kama timu tunatakiwa tuwe na mpango B au tunajitayarisha kwa chochote ambacho kinatokeza. Tutaathirika lakini nafikiri ni fursa kwa wachezaji wengine ambao watapata nafasi kuweza kuitumia vizuri na naamini tunao vijana ambao wanakuja vizuri,” amesema kocha wa Taifa Stars, Hemed Morocco.

Samatta amekuwa moto wa kuotea mbali kwenye kikosi cha PAOK katika siku za hivi karibuni ambapo kabla ya kuumia goti, alihusika na mabao sita katika mechi tano za ligi za timu hiyo akifunga manne na kupiga pasi mbili za mwisho.

Ni kikosi ambacho kina sura nyingi zilizorejea kundi baada ya kukosa uteuzi katika nyakati kadhaa ambazo timu hiyo ilikuwa na majukumu ya mashindano ya kimataifa.

Nyota wa Newcastle Jets ya Australia, Charles M’mombwa amekuwa miongoni mwa nyota walioitwa baada ya kukosa mechi kadhaa kama ilivyo kwa beki wa Salford City ya England, Haji Mnoga.

Mwingine aliyerejea kikosini ni kipa wa Simba, Ally Salim anayechukua nafasi ya Aishi Manula ambaye hajajumuishwa kikosini pia kuna urejeo wa Selemani Mwalimu wa Wydad Casablanca.

Kuna sura tatu mpya kikosini ambazo ni makipa Yakoub Suleiman wa JKT Tanzania na Hussein Masaranga wa Singida Black Stars lakini pia kuna beki wa kushoto wa Coastal Union, Miraji Abdallah.

Wachezaji 24 wanaounda kikosi cha Taifa Stars ni Ally Salim, Yakoub Suleiman, Hussein Masaranga, Shomari Kapombe, Lusajo Mwaikenda, Mohammed Hussein, Pascal Msindo, Miraji Abdallah, Ibrahim Abdullah, Dickson Job, Abdulrazack Hamza, Ibrahim Ame na Haji Mnoga.

Wengine ni Novatus Miroshi, Mudathir Yahya, Yusuph Kagoma, Feisal Salum, Charles M’mombwa, Kibu Denis, Simon Msuva, Clement Mzize, Iddy Selemani, Selemani Mwalimu na Kelvin John.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *