
Urusi na Marekani zimeanza mazungumzo nchini Saudi Arabia siku ya Jumatatu kujadili uwezekano wa kupatikana kwa usitishwaji vita nchini Ukraine, shirika la habari la Urusi TASS limeripoti, likinukuu chanzo kilicho karibu na mazungumzo hayo.
Imechapishwa:
Dakika 2
Matangazo ya kibiashara
Urusi na Marekani zinakutana nchini Saudi Arabia Jumatatu hii kwa mazungumzo ambayo Kremlin imeyataja mara moja kuwa “magumu.” Lengo: kuanzisha usiishwaji vita ambao si kamili nchini Ukraine baada ya zaidi ya miaka mitatu ya mashambulizi ya Urusi. Rais wa Marekani Donald Trump, ambaye uhusiano wake na Vladimir Putin umebadilisha kadi za mzozo huo, anadai kutaka kumaliza uhasama na ametuma wajumbe wake Riyadh kwa mazungumzo na pande zote mbili.
Ujumbe wa Urusi, unaojumuisha seneta na mwanadiplomasia wa zamani Grigory Karasin, na Sergei Beseda, mwanachama mkuu wa FSB, idara ya usalama, wamekutana na ujumbe wa Marekani katika Hoteli ya Ritz-Carlton huko Riyadh, chanzo hicho kimesema.
Tovuti za habari za upotoshaji juu ya Ukraine ni tishio kwa uaminifu wa vyombo vya habari
Tovuti za Urusi zinazojifanya kama tovuti za habari, lakini kwa hakika zinaeneza habari potofu kuhusu Ukraine, zinaongezeka, kwa lengo la kudhoofisha imani ya umma katika vyombo vya habari halisi, watafiti wanaonya.
Mapema mwezi huu, Clear Story News iliripoti habari za uongo kwamba Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky anatumia pesa za Marekani kuwalipa waandishi wa habari wa nchi za Magharibi kumkosoa Donald Trump. “Makala” haya yalionyeshwa kwa taswira ya barua inayodaiwa kutumwa na Volodymyr Zelensky kwa spika wa bunge la Ukraine, akiomba “mpango” wa “kujenga taswira mbaya” ya rais wa Marekani utekelezwe. Kulingana na NewsGuard, shirika linalohusika na kupambana na taarifa potofu na kutumia programu ya uthibitishaji wa InVID, barua hiyo ni ghushi, kwani muhuri wa rais na sahihi ya Volodymyr Zelensky zimebadilishwa kidijitali. Pia kulingana na NewsGuard, Clear Story News ni tovuti iliyoathiriwa na Urusi iliyounganishwa na John Mark Dougan, mwanaharakati wa Kimarekani anayeunga mkono Kremlin. “Makala” hayo yalichapishwa wiki moja baadaye kwenye tovuti nyingine inayounga mkono Urusi, USATimes.news.
Mashambulio mapya ya Urusi usiku kucha
Licha ya kuharakishwa kwa juhudi za kupatanisha maoni ya pande zinazozozana juu ya njia za kufikia usitishaji mapigano, mapigano yanaendelea na mashambulizi mabaya nchini Ukraine na Urusi. Mamlaka ya Ukraine imeripoti mashambuliz usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu ambayo yamelenga mikoa ya Kyiv, Kharkiv (mashariki) na Zaporizhzhia (mashariki), na kusababisha watu kadhaa kujeruhiwa, siku moja baada ya milipuko mibaya ya mabomu kwenye mji mkuu.
Jeshi la Ukraine pia lilitangaza siku ya Jumapili kwamba limekitwaa tena kijiji kidogo cha Nadia, katika eneo la mashariki la Lugansk, mafanikio adimu kwa wanajeshi wa Ukraine katika eneo hili ambalo karibu kabisa kudhibitiwa na Urusi. Vikosi vya Urusi vilisema vimeuteka mji wa Sribne, pia mashariki mwa Ukraine.