Mazungumzo ya moja kwa moja na waasi wa M23 kufanyika Machi 18 : Angola

Angola imetangaza jana jioni katika taarifa ya ikulu ya rais kwamba mazungumzo ya amani ya moja kwa moja yatafanyika Jumanne, Machi 18, mjini Luanda kati ya wajumbe kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na wajumbe wa AFC/ M23.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumanne, marais wa Kongo na Angola Felix Tshisekedi na Joao Lourenço walikutana mjini Luanda. Ilikuwa baada ya mkutano huu ambapo Angola, ambayo ni mpatanishi katika mgogoro huu, ilitangaza nia yake ya kuanzisha mazungumzo kati ya Kinshasa na kundi la waasi la AFC/M23. Lakini tangazo hilo linazua maswali. Ofisi ya rais wa Kongo ilithibitisha Jumatano jioni kwamba imepokea mwaliko.

Duru za awali za mazungumzo ya amani yaliyosimamiwa na Angola yameshindwa kusitisha mapigano kati ya jeshi la Kongo na M23, katika eneo lenye hali tete la DRC linalokabiliwa na mapigano kati ya makundi mbalimbali yenye silaha.

Lakini siku ya Jumanne, Angola ilisema pande hizo mbili zilikubaliana kuja kwenye meza ya mazungumzo, baada ya Rais wa Kongo Felix Tshisekedi kujadili mzozo huo na mwenzake wa Angola Joao Lourenco.

“Kufuatia hatua zilizochukuliwa na upatanishi wa Angola … wajumbe kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na M23 wataanza mazungumzo ya moja kwa moja ya amani mnamo Machi 18 katika mji wa Luanda,” ofisi ya rais wa Angola ilisema katika taarifa yake jana jioni.

Tshisekedi hapo awali alikataa kufanya mazungumzo na M23, ambayo imefanya mashambulizi makubwa mashariki mwa DRC kwa kuungwa mkono na Rwanda.

Rais wa DRC Felix Tshisekedi awali alikuwa ameshikilia msimamo wa kutofanya mazungumzo na waasi wa M23.
Rais wa DRC Felix Tshisekedi awali alikuwa ameshikilia msimamo wa kutofanya mazungumzo na waasi wa M23. via REUTERS – Christophe Ena

Katika chapisho kwenye X, kiongozi wa M23 Bertrand Bisimwa alijigamba kwamba wamefaulu kumlazimisha Tshisekedi kwenye meza ya mazungumzo, na kuliita “chaguo pekee la kistaarabu la kutatua mgogoro uliopo”.

Hayo yanajiri wakati viongoezi wa jumuiya ya SADC wanakutana alhamisi hii kujalidi mgogoro wa DRC.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *