Mazungumzo ya Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Iran na Yemen kuhusu matukio ya eneo

Sayyid Abbas Araqchi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, amefanya mazungumzo ya simu na Jamal Ahmed Ali Amer, Waziri wa Mambo ya Nje na Wahamiaji wa Jamhuri ya Yemen, na kusisitiza kuendelea kwa msaada wa Iran kwa serikali na watu wa Yemen.