Sasa ni rasmi kuwa Mazungumzo ya kurejesha amani Sudan Kusini yanayojulikana kama Tumaini, yamevunjika mjini Nairobi. Haijulikani ni lini mazungumzo hayo yatarelewa tena.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Pagan Amum, kiongozi wa vyama vya kisiasa vya upinzani Sudan kusini na pia kiongozi wa kundi la kiisiasa la Real Sudan People’s Liberation Movement, anatueleza jinsi mazungumzo hayo ya kurejesha amani Sudan Kusini, yalivyovunjika.
‘‘Wakati tulipokuwa tukiendelea na mazungumzo kwa ghafla serikali ya Sudan kusini ilitujulisha rasmi kuwa ilikuwa inajiondoa kwenye mazungmzo hayo. Hivyo ndivyo mazungumzo yalivunjika hata tulipojaribu kutoa mapendekezo ya mwisho, serikali haikutaka kusikia tulichokuwa tukisema. Kilichobaki sasa ni kwa wananchi wa Sudan kusini kuendelea na mapambano ili kuwepo na amani ya kudumu na serikali nzuri thabiti.’’ Alisema Pagan Amum, kiongozi wa vyama vya kisiasa vya upinzani Sudan kusini.

Mohamed Ali Guyo, naibu wa mwakilishi mkuu wa serikali ya Sudan Kusini na naibu wa mpatanishi katika mazungumzo ya Nairobi, alikuwa na ujumbe huu kutoka mji mkuu Juba.
‘‘Serikali ya Sudan kusini imeomba kuahirishwa kwa muda kwa mazungumzo kutoa nafasi kwetu wawakilishi kurudi Juba kupata mashauri zaidi. Kwa sasa mazungumzo yamepiga hatua mazungumzo hayo yanayojulikana kama msukumo wa Tumaini yangali na lengo la kuleta amani ya kudumu kwa watu wotewa Sudan Kusini.’’ alieleza Mohamed Ali Guyo.
Hii ni mara ya tatu tangu tangu mwezi wa tano mwaka jana kwa mazungumzo hayo ya kurejesha amani Sudan Kusini kuvuvunjika.
James Shimanyula- Sudan Kusini.